SAUTFM

Friday 3 June 2016

MUHAMMAD ALI AFARIKI DUNIA

Bingwa za zamani wa uzito wa juu Muhammad Ali "the greatest" amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Phoenix  alipolazwa kuanzia juzi akisumbuliwa na matatizo ya mfumo wa upumuaji.Muhammad ambaye alizaliwa mwaka 1924 amefariki akiwa na miaka 74.

Thursday 2 June 2016

KESI YA MESSI KUSIKILIZWA LEO

Mchezaji wa Argentina na klabu ya Barcelona Lionel Messi  anatarajia kutoa ushahidi  katika mahakama ya Hispania kutokana na kesi inayomkabili ya kukwepa kulipa kodi.
Messi na baba yake anaejulikana kwa jina la Jorge mbaye anamsimamia maswala ya kiuchumi ya mchezaji huyo wanatuumiwa kukwepa kulipa kodi nchini Hispania ya zaidi euro msillion 4 kati  ya mwaka 2007 na 2009 
Uongozi umedai kuwa Messi na baba yake walitumia taasisi za kutakatisha fedha kufuta mapato ambayo waliyapata kutoka haki miliki za picha,
Wasimamizi wa kodi nchini humo wanataka watuhumiwa hao walipe faini kubwa  na  kifungo  lakini wawili hao wamekuwa wakikanusha makosa hayo,.
Kesi hiyo ilianza kusikilizwa siku ya jumanne na inatarajwia hukumu kutolewa hii leolakini uamuzi huo unaweza usitolewe leo mpaka wiki ijayo.
Kutokana na kesi hiyo Messi amekosa sehemu ya maandalizi ya timu ya taifa ambayo inajiandaa naa michuano ya Kopa Amerca inayotarajia kuanza ijumaa hii huko America,Mechi ya kwanza ya Argentina itachezwa Jumatatu ya tarehe 6 mwezi huu.

Ushahidi wa kesi hiyo utahusisha muonekano halisi wa messi ikihusisha mikataba mbalimbali inayomdhamini kama  Banco Sabadell, Danone, Adidas, Pepsi-Cola, Procter na Gamble, na kampuni ya chakula ya kuwaiti

DI MATTEO MENEJA MPYA ASTON VILLA

Klabu ya Aston Villa leo imemtangaza muitaliano Robert Di Matteo kuwa meneja wao mpya huku mchezaji mwenzake wa zamani wa klabu ya chelsea Steve Clarke akiwa msaidizi wake.Mameneja hao hawajawahi kufanya kazi pamoja ila wamewahi kucheza pamoja kwa miaka miwili katika klabu ya chelsea wanakazi nzito ya kuirudisha klabu hiyo kwenye ubora wake baada ya kuwa chini ya kiwango

KAKA AONDOLEWA KWENYE KIKOSI CHA BRAZIL

Ricardo kaka ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kinachoshiriki michuano ya Copa America kutokana na majeruhi na Paul Ganso amechukua nafasi yake.Kaka ambaye alichukua nafasi ya mchezaji wa Bayern Munich Douglas Costa baada ya kuumia pia michezoni. 

GUNDOGAN RASMI MANCHESTER CITY

Klabu ya Manchester city imetangaza kumsajili kiungo mjerumani Ilkay Gundogan kutoka katika klabu ya Borussia Dortmund kwa mkataba wa miaka minne huku ikilipotiwa kuwa paundi milioni 20 zimetumika kwenye usajili huo.Kiungo huyo mwenye miaka 25 ambaye anatarajiwa kukosa michuano ya Euro 2016 na mechi za mwanzoni za ligi amekuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha mpya wa Manchester City Pep Guardiola.

Wednesday 1 June 2016

MAGAZETINI LEO

KURASA ZA MBELE ZA MAGAZETI MBALIMBALI LEO ALHAMISI,JUNE 2





















Friday 27 May 2016

KAKA AITWA TIMU YA TAIFA

Ricardo Kaka ameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil baada ya mchezaji wa Bayern Munich Douglas Costa kuumia.Brazil wanajiandaa na michuano ya copa america inayotarajiwa kuanza mwezi ujao.